ISAKA MUTU MUKONGWE — Cantiques EUJC

N° 542

ISAKA MUTU MUKONGWE

1.

Isaka mutu mukongwe macho ikapofuka akaomba mwanaye Esau nyama yenyi kunona amuongezee furaha (X2)

Refrain

Kweli Yakobo wangu nenda uchukuwe mwana mbuzi uje upokee Baraka

Baraka mu Neno nenda uchukuwe mwana mbuzi uje upokee Baraka

Kweli Yakobo wangu ee nenda uchukuwe mwana mbuzi uje upokee Baraka

Usikawe njiani nenda uchukuwe mwana mbuzi uje upokee Baraka

Baraka mu Neno nenda uchukuwe mwana mbuzi uje upokee Baraka

2.

Rebeka akatayarisha wana mbuzi wawili akampa Yakobo amupelekeye Isaka amuongezee furaha (X2).

3.

Esau akachukizwa akalia akaomboleza juu yangu nitauwa Yakobo ameni nyanganya furaha (X2).