WAKATUPA DANIELI PANGONI MWA SIMBA — Cantiques EUJC

N° 561

WAKATUPA DANIELI PANGONI MWA SIMBA

1.

Wakatupa Danieli pangoni mwa simba kwani alikuwa mufanya kazi wa Mungu wa Uzima « kili siku kila siku mara tatu » chumba chake cha juu ma dirisha uangalia mu Yerusalema (X2).

Refrain

Danieli Danieli wewe pangoni mwa simba (X2)

Tazama Danieli simba aikumula yoyoyo kwa jina la mufalme

Tazama kerubi kerubi la mufalme kafunga ee simba

2.

Ili ni neno la mufalme Dario, Mungu wa Danieli aimidiwe, musiwe miungu mingine inchini mwangu, kwani Mungu wa Danieli anauweza wote « Atakuokowa pangoni mwa simba, atakuokowa mu mambo ya duniani » (X2)

3.

Wakija na jambo la duniani kwa wewe mujoli (X2) « (basi wewe) ujuwe Neno la Mungu unalo » (X2)

Litakuokowa pangoni mwa simba, Neno la Bwana litakuokowa mu mambo ya duniani (X2).