N° 566
HUDUMA ZOTE ZA DUNIANI
Huduma zote za duniani « (huduma) hazikose torati ndani yake ». Hivi Mungu kamupatia Musa (Musa) sheria hizo nendeni munihudumie
Mungu akanena kwa sharia hizo nitazigawa yoyoyo sehemu hizi mbili :
« Umupenda Bwana Mungu kwa moyo wako wote
Umupenda jirani yako kwa nafsi yako yote ».
Naomi naye akanena, Naomi naye akanena ewe Rutu wangu nimekwisha kuwa mukongwe « rejeeni nyumbani mwa wazazi (mujoli wangu) »
Mimi sina na vya kukulisha rejeeni nyumbani mwa wazazi
Mimi sina na wanaume rejeeni nyumbani mwa wazazi
Mimi sina na vya kukuvika rejeeni nyumbani mwa wazazi
Mimi sina na A, ee rejeeni nyumbani mwa wazazi
Rutu akaomboleza, Rutu akaomboleza ewe mamangu sita kuacha kamwe, nitajilaza mahali ulalapo
Nitaketi mahali uketipo
Nitavaa chochote uvaacho
Mungu atatujalia chochote uombacho
Mungu wako aliye hai ni wangu pia, atatukirimia wokovu, atatupa uzima wa milele.