TUMEVUKA LEO BAHARI KUBWA — Cantiques EUJC

N° 586

TUMEVUKA LEO BAHARI KUBWA

1.

Tumevuka leo bahari kubwa kwelekea Kanana inchi ya amani “Farao na majeshi yake yote wamekufa baharini” njooni twende (X2).

Refrain

Wenye kulala mulamuke wenye kuketi musimame vita yatungoja mbele yetu ili tukazingie Kanana inchi ya wateule wajoli twende (X2)

Kwa kuriti Kanana twende yoyo twende Kanana

Tupigane vita twende yoyo twende Kanana

Tushikeni ngao twende yoyo twende Kanana

Ya kushika mishaletwende yoyo twende Kanana

2.

Tuwe na imani yenye ufahamu na hakikisho tusiwe wajinga katika akili zetu “(bayana) bayana ya kila jambo wajoli katika Neno la Mungu” tusiwe mateka (X2)

3.

Jiazarini mwenzangu tusiwe mu muji wowote muji ni kitu kibaya, tusibakie njiani tusiwe mateka.

“Miji eh eh miji eh” miji ni kitu kibaya iliuwisha Yoane wa Mungu kwa Herode mufalme eh “kweli Yoane wetu akafa yoyoyo kwa ajili ya miji”

Commentaire

Miji ya kupenda kula akafa yoyoyo kwa ajili ya miji

Miji ya kugusagusa akafa yoyoyo kwa ajili ya miji, …