EWE MALAIKA WA NURU — Cantiques EUJC

N° 9

EWE MALAIKA WA NURU

1.

Ewe malaika wa nuru , ewe nyota alfajiri lusifero ulipendwa sana kuko bwana mumba wako "Akakuvika mawe ya bei lulu ya damani kubwa~2x

Refrain

Uchuruzi wako ulikujaza uzalimu toka katikati ya mawe ya moto wewe ulitenda zambi , lucifero ulinena kwamba nitapaa juu mbinguni kuliko mulima wa mungu, lucifero ulinena kwamba nitapaa juu mbinguni kuliko nyota za bwana.

2.

Mawe ya bei lusifero uliyo vikua tazama : kiki nyekundu, yakuti ya manjano, ulivikua na alimasi, zabara jadi, zumaridi na ya aspi, bahara mani, shoamu na zahzbu.

3.

Vita kutoka mbinguni Mikaeli na jeshi lake kupigana na yule shetani na kundi lake lote Diabolo akatupua chini na kundi lake lote, furahini ninyi mbingu pia na malaika wote ole wenu duniani na waishio ndani ya bahari, furahini ninyi watu waishimo mu neno la mungu.